- Haifai kwa mwanamke kusafiri bila maharim.
- Mwanamke hawezi kuwa maharim wa mwanamke mwenzie katika safari; kwa kauli yake: "Mume wake, au aliyeharamu kwake kumuoa (Maharim)"
- Kila inayoitwa safari basi mwanamke anakatazwa kusafiri bila mume wake au maharim yake, na hadithi ilikuwa kulinga na hali ya muulizaji na mji wake.
- Maharim wa mwanamke ni mume wake au aliyeharamu kwake kumuoa kwa uharamu wa moja kwa moja, kwa sababu ya udugu wa damu, kama baba na mtoto na baba mdogo au mkubwa na mjomba, au kwa kunyonya, kama baba wa kunyonya au baba mdogo wa kunyonya, au ukwe kama baba mkwe, na anatakiwa awe muislamu aliyebaleghe, mwaminifu, kwani lengo la maharim ni kumlinda mwanamke na kumchunga na kumjali katika mambo yake.
- Sheria imempa kipaumbele mwanamke, na imemhami na kumlinda.
- Haikubaliki swala ya sunna isiyokuwa na sababu, baada ya swala ya Alfajiri na Lasiri, na haingii hapa kulipa swala ya faradhi iliyopita, na zenye sababu, kama salamu ya msikiti na mfano wake.
- Uharamu wa kusali mara tu baada ya kuchomoza Jua, bali ni lazima linyanyuke kiasi cha mkuki, kwa takribani kama dakika kumi (10) mpaka robo saa hivi.
- Wakati wa Lasiri unakwenda mpaka kuzama Jua.
- Ndani ya hadithi kuna kufaa kufunga safari kwenda katika misikiti mitatu.
- Fadhila na ubora wa misikiti mitatu, na tofauti yake kwa misikiti mingine.
- Hairuhusiwi kusafiri kwenda kufanya ziara ya makaburi, hata kama ni kaburi la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, ila inafaa kulitembelea kwa anayeishi Madina, au akalifikia kwa lengo la kisheria au lengo linalofaa.