Atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakufanya matendo mabaya,na hakufanya uwovu, atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakaye hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hakufanya matendo mabaya,na hakufanya uwovu, atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake"
Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Ufafanuzi
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye hiji kwa kutaka radhi za Allah Mtukufu na akawa hakufanya yasiyofaa; Na yasiyofaa hapa maana yake ni tendo la ndoa na vitangulizi vyake, kama busu, kugusana, neno hili hutumika pia kumaanisha maneno machafu, na akawa hakufanya uovu; kwa kufanya maasi na madhambi, Na miongoni mwa uovu ni kufanya makatazo ya ihiramu (Hija), atarudi kutoka katika hija yake akiwa kasamehewa, kama azaliwavyo mtoto akiwa amesalimika kutokana na madhambi.
Hadeeth benefits
Uwovu pamoja na kuwa umekatazwa katika hali zote, katazo hilo linatiwa mkazo katika Hija kwa kuheshimu na kutukuza ibada ya Hija.
Mwanadamu huzaliwa pasina kuwa na makosa akiwa kaepukana na madhambi; hivyo hawezi kubeba madhambi ya mwingine.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others