- Uharamu wa kufunga siku mbili za Iddil-Fitiri na Iddil-Adh-ha, na siku tatu za kubanika nyama; kwa sababu zinafuatana na siku ya Iddil-Adh-ha isipokuwa kwa yule ambaye hakupata cha kutoa, itafaa kwake kufunga siku za kubanika nyama.
- Amesema bin Hajari: Imesemekana kuwa: Na faida ya kuzitaja siku mbili ni ishara ya kuonyesha sababu ya uwajibu wa kufungua ndani yake, nazo ndio mapumziko ya swaumu, na kudhihirisha ukamilifu wake peke yake kwa kufungua siku zilizo baada yake, na Idd nyingine ni kwa ajili ya kuchinja kwa mwenye kujikurubisha kwa kichinjwa chake ili ale kutoka katika kichinjwa hicho.
- Inapendeza kwa mtoa hotuba ataje katika hotuba yake yale yanayohusiana na wakati wake miongoni mwa hukumu, na atumie fursa ya matukio kama hayo.
- Sheria ya kula kutoka katika kichinjwa cha ibada.