Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema kati ya sijida mbili: "Allaahumma ghfir lii, warhamnii, wa aafiniii, wahdinii, warzuqniii
Imepokewa Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema kati ya sijida mbili: "Allaahumma ghfir lii, warhamnii, wa aafiniii, wahdinii, warzuqniii".
Ufafanuzi
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiomba kati ya sijida mbili katika sala yake kwa dua hizi tano ambazo muislamu anazihitajia kwa uhitaji mkubwa, na zimekusanya heri za dunia na akhera, ikiwemo kuomba msamaha na stara ya madhambi na kufutwa kwake, na kumiminiwa rehema, na kusalimishwa na mambo yenye utata na matamanio na maradhi na magonjwa, na kumuomba Allah uongofu katika haki na kudumu katika hilo, na kupewa imani na elimu na matendo mema, na mali nzuri ya halali.
Hadeeth benefits
Sheria ya kuomba dua hii katika kikao kati ya sijida mbili.
Ubora wa dua hizi kwa kukusanya heri za dunia na akhera.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others