- Muislamu anahimizwa kumtaja Mwenyezi Mungu mwisho wa usiku.
- Nyakati zinazidiana ubora kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu na kuomba dua na kuswali.
- Amesema Muraik: Katika tofauti baina ya kusema kwake: “Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja,” na kusema kwake: “Mahala pa karibu zaidi anapokuwa mja na Mola wake Mlezi ni pale anapokuwa kasujudu”: Kinachokusudiwa hapa ni kuashiria wakati ambapo Mola anakuwa karibu zaidi na mja, yaani katikati ya usiku, na kinachokusudiwa hapo ni kueleza hali ya ukaribu wa mja na Mola ni pale anapokuwa katika hali ya kusujudu.