- Katika hekima za kunyanyua mikono ndani ya swala, ni pambo la swala, na ni kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Imethibiti kutoka kwake rehema na amani ziwe juu yake, kuwa alinyanyua mikono yake katika nafasi ya nne, kama ilivyokuja katika riwaya ya Abuu Humaid Al-Sa'idi kwa Abuu Daudi na wengineo, ambayo ni wakati wa kusimama kutoka tashahudi ya kwanza. katika swala ya rakaa tatu na nne.
- Imethibiti vile vile kutoka kwake rehema na amani zimshukie, pia alikuwa akinyanyua mikono yake usawa wa masikio yake bila ya kuyagusa, kama ilivyo katika riwaya ya Maliki bin Al-Huwairith katika Sahihi mbili: “Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie, alikuwa akinyanyua mikono yake mpaka inalingana na masikio yake.”
- Na kukusanya kati ya kusema: "Sami'allaahu liman hamidah, na kusema: "Rabbanaa walakal hamdu, hii ni maalumu kwa Imamu na anayeswali peke yake, ama maamuma yeye atasema: Rabbanaa walakal hamdu, pekee.
- Kusema: Rabbanaa walakal hamdu “Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako” baada ya kurukuu ni sahihi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kuna namna nne, na hii ni mojawapo, na ni bora kwa mtu afuatilie namna hizi zote, ili wakati mwingine analeta hii, na wakati mwingine analeta hii.