- Haikubaliki kusoma sura isiyokuwa suratul Fatiha ikiwa ana uwezo wa kuisoma.
- Kuharibika kwa rakaa ambayo haikusomwa ndani yake suratul fatiha, kwa mwenye kufanya kusudi na mjinga na aliyesahau; kwa sababu ni nguzo, na nguzo huwa hazidondoki kwa hali yoyote ile.
- Kisoma cha Suratul Fatiha kinaondoka kwa maamuma anapomkuta imam karukuu.