Kutoka kwa Salim bin Abil Ja'di amesema: Mtu mmoja alisema: Laiti ningeswali nikastarehe, wakawa kana kwamba wamelitia dosari hilo, akasema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ewe Bilali, simamisha swala, tupe raha kwayo".
Imepokelewa na Abuu Daud
Ufafanuzi
Akasema mtu mmoja katika Masahaba: Laiti ningeliswali nikastarehe, waliokuwa naye waka kana kwamba wamemuabisha kwa hilo, akasema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Ewe Bilali! Nyanyua adhana na simamisha swala; ilitustarehe kwayo; na hii ni kwa sababu ndani yake kuna kuzungumza na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na raha ya roho na moyo.
Hadeeth benefits
Raha ya moyo iko ndani ya swala; kwani ndani yake kuna kuzungumza na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kemeo kwa mvivu katika ibada.
Atakayetekeleza wajibu ulio juu yake, na akajiweka mbali na dhima, atapata raha kwa ibada hiyo na atahisi utulivu.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others