Hakuna swala chakula kinapokuwa tayari, na wala hakuna (swala) akiwa anazuia na kubana vichafu viwili(Haja kubwa na ndogo)
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna swala chakula kinapokuwa tayari, na wala hakuna (swala) akiwa anazuia na kubana vichafu viwili(Haja kubwa na ndogo)".
Imepokelewa na Imamu Muslim
Ufafanuzi
Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuswali kinapotengwa chakula kile anachokitamani mwenye kuswali, na moyo wake umefungamana nacho.
Na vile vile amekataza kuswali mtu akiwa anazuia haja mbili -nazo ni mkojo na haja kubwa-, kwakuwa atashughulika na kuzuia udhia.
Hadeeth benefits
Ni lazima kwa mwenye kusali aweke mbali kila chenye kumshughulisha katika swala yake kabla ya kuingia ndani ya swala.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others