- Ni karaha kuacha kusimama usiku, nakuwa hilo ni kwa sababu ya Shetani.
- Kutahadhari na Shetani anayemkalia mwanadam katika njia zote; ili amkinge na kuzuia kati yake na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Amesema bin Hajari: Kauli yake: "Hakusimama kuswali" Makusudio yake ni aina ya sala, na inawezekana kuwa ni ahadi, na inakusudiwa ni swala ya usiku au swala ya faradhi.
- Amesema Twaibi: Limetajwa sikio pekee, japokuwa jicho ndio linastahiki zaidi kulala ikiwa ni ishara ya uzito wa usingizi, kwa sababu masikio ndio nyenzo za umakini, na umetajwa mkojo; kwa sababu ndio mwepesi kupenya katika njia za sikio, na mwepesi kutembea katika mishipa, na kusababisha uvivu katika viungo vyote.