- Maamuma anapokuwa na imam kuna hali nne: haliTatu zimekatazwa, nazo ni: Kumtangulia, na kwenda naye sawa, na kuchelewa, na mafundisho kwa maamuma: Ni kumfuata imam.
- Ulazima wa maamuma kumfuata imam ndani ya swala.
- Ahadi ya adhabu ya kubadilika sura kwa atakayenyanyua kichwa chake kabla ya imam na kuwa sura ya punda ni jambo linawezekana, nako ni kufutwa kwa sura halisi.