/ Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja akiswali peke yake nyuma ya safu, akamuamrisha arudie swala yake

Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja akiswali peke yake nyuma ya safu, akamuamrisha arudie swala yake

Kutoka kwa Waabiswa radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja akiswali peke yake nyuma ya safu, akamuamrisha arudie swala yake.

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja aliyeswali nyuma ya safu peke yake, akamuamrisha arudie swala yake; kwa sababu swala yake haikusihi kwa hali hii.

Hadeeth benefits

  1. Himizo la kuwahi swala ya jamaa na kuwahi mbele kwa ajili yake, na asiswali nyuma ya safu peke yake ili swala yake asiitie katika kubatilika
  2. Amesema bin Hajari: Atakayeanza swala peke yake nyuma ya safu kisha akaingia katika safu kabla ya kunyanyuka kutoka katika rukuu, hatolazimika kurudia, kama ilivyokuja katika hadithi ya Abiibakra, na vinginevyo itakuwa wajibu kwa mujibu wa ujumla wa hadithi ya Waabiswa.