- Mwenye kuswali akiitilia shaka swala yake na akawa hakupata ufumbuzi wa moja kati ya mambo mawili, basi aondoe shaka na afanyie kazi uhakika, ambao ni uchache, basi atatimiza swala yake na atasujudu kwa ajili ya kusahau kabla hajatoa salamu kisha atatoa salamu.
- Sijida hizi mbili ni njia ya kurekebisha swala, na kumrudisha Shetani katika hali ya udhalili na unyonge, mbali na alichotaka.
- Shaka iliyoko katika Hadithi ni kusitasita bila ya kupata majibu, hivyo ikipatikana dhana na akapata majibu basi atafanyia kazi dhana yake.
- Himizo la kupambana na wasi wasi na kuuzuia kwa kutekeleza amri ya sheria.