- Sunna ya kudumu na adhkari za baada ya swala za faradhi.
- Muislamu hujifaharisha kwa dini yake, na hudhihirisha nembo zake, hata kama makafiri watachukia.
- Linapokuja katika hadithi neno: "Mwisho wa swala", Ikiwa kilichotajwa ndani ya hadithi ni dhikri, basi asili yake hapa ni baada ya salamu, na ikiwa ni dua inakuwa kabla ya salamu ndani ya swala.