- Fadhila za swaumu nakuwa inamuhifadhi mfungaji katika dunia kutokana na matamanio, na Akhera kutokana na adhabu ya Moto.
- Miongoni mwa adabu za swaumu ni kuacha maneno mabaya na ya hovyo, na kusubiri dhidi ya maudhi ya watu na kukabiliana na maudhi hayo kwa subira na ihisani.
- Swaumu au mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu anapofurahi kwa sababu ya kukamilisha ibada yake na kuimaliza hilo halipunguzi malipo yake Akhera.
- Furaha kamili inakuwa kwa kukutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu, pale wanapotimiziwa wenye subira na wafungaji malipo yao pasina hesabu.
- Kuwafahamisha watu kwa ibada uliyonayo wakati wa haja na masilahi si katika riyaa kwa kauli yake: "Hakika mimi nimefunga".
- Mfungaji iliyekamilika swaumu yake ni yule viliyefunga viungo vyake kutokana na madhambi, na ulimi wake kutokana na uongo na machafu, na kusema uongo, na tumbo lake kutokana na chakula na vinywaji.
- Katazo la kufanya fujo na ugomvi na zogo wakati wa swaumu limetiwa mkazo, lakini pia yamekatazwa hayo kwa mtu asiyekuwa katika swaumu.
- Hadithi hii ni katika yale anayoyapokea Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithi ya kiuungu, nayo ni ile ambayo matamshi yake na maana yake imetoka kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa haina mambo maalumu kama ya Qur'ani ambayo inatofautiana kwayo na maneno mengine, ikiwemo kukitumia kisomo chake kama ibada na kuwa twahara (msafi) na kutoa changamoto na maswala kisayansi na mengineyo.