- Mali iliyoko mikononi mwa watu ni mali ya Mwenyezi Mungu, amewamilikisha ili waitoe katika njia za kisheria, na waepuke kuitumia katika batili, na hii inawahusu viongozi na wasiokuwa viongozi.
- Sheria imetia mkazo katika mali ya umma, nakuwa yeyote atakayesimamia chochote basi atambue kuwa atahesabiwa juu ya ukusanyaji wake na matumizi yake.
- Anaingia katika ahadi hii ya adhabu mwenye kufanya matumizi yasiyokuwa ya kisheria katika mali, sawa sawa iwe ni mali yake, au mali ya mwingine.