- Himizo la kutoa sadaka na kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.
- Kutoa katika njia za heri ni miongoni mwa sababu kubwa za kupata baraka katika riziki na kuzidishwa kwake, na Mwenyezi Mungu kumpa badala mja katika kile alichokitoa.
- Hadithi hii ni katika zile anazozipokea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithil Qudsi au Hadithil Ilahi, nayo ni ile ambayo tamko lake na maana yake inatoka kwa Allah, isipokuwa haina upekee kama wa Qur'ani inaojipambanua nayo kwa vingine, ikiwa kisomo chake kutumika katika ibada, na kuwa twahara kabla ya kusoma, na kuwashinda watu kwa changamoto zake, na mengineyo.