- Ukamilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika dhati yake, na sifa zake, na vitendo vyake, na hukumu zake.
- Amri ya kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa kumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Kutumia maneno yenye kuhamasisha kufanya matendo, kiasi kwamba alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha Mitume", anapojua muumini kuwa hili ni katika yale waliyoamrishwa Mitume basi anapata nguvu na anahamasika kulitekeleza.
- Katika vizuizi vya kujibiwa dua ni kula vya haramu.
- Katika sababu za kujibiwa dua ni mambo matano: La kwanza: Kuwa na safari ndefu, kwakuwa ndani yake kuna kudhoofika, ambayo ni miongoni mwa sababu kubwa za kujibiwa. La pili: Wakati wa kudharurika. La tatu: kunyoosha mikono kuelekea mbinguni. La nne: Kung'ang'ania kwa Mwenyezi Mungu kwa kurudiarudia kusema ewe Mola Mlezi, na ni katika maneno makubwa ambayo hutumika kwa lengo la kutaka kujibiwa. La tano: Kula chakula kizuri na vinywaji vizuri.
- Kula halali nzuri ni katika sababu zinazosaidia kutenda amali njema.
- Amesema Kadhi: Kizuri ni kinyume cha kibaya, akisifiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi hukusudiwa kuwa ametakasika na mapungufu, na ametukuka hana maafa, na akisifiwa mja moja kwa moja basi hukusudiwa kuwa hana tabia chafu na matendo mabaya, na anajipamba na kinyume cha hayo, na ikisifiwa mali basi hukusudiwa inapokuwa ya halali katika mali bora.