- Wamekubaliana wanachuoni kuwa katika mambo yanayomfuata mwanadam baada ya kufa kwake katika thawabu ni: Sadaka ya kuendelea, na elimu yenye kunufaisha watu, na dua, na imekuja Hija katika hadithi zingine pia.
- Yametajwa mambo haya matatu pekee katika hadithi; kwa sababu ndio msingi wa mambo ya kheri, na ndio mambo wanayoyafanya watu wema wengi baada ya kuondoka kwao.
- Kila elimu yenye kunufaisha basi hupatikana malipo kwa elimu hiyo, lakini kilele chake ni elimu ya kisheria na elimu za msingi kwake.
- Elimu ndiyo yenye manufaa zaidi kati ya haya matatu; Kwa sababu elimu inamnufaisha mtu anayeisoma, elimu inahusisha kuihifadhi Sheria, inawanufaisha watu kwa ujumla, na ni pana zaidi na ni ya jumla, kwa sababu anajifunza kutoka katika elimu yako aliyepo wakati wa uhai wako na atakayekuwepo baada ya kufa kwako.
- Himizo la kulea watoto wema; Wao ndio wanaowanufaisha wazazi wao Akhera, na miongoni mwa manufaa yao ni kuwaombea dua.
- Himizo la kuwatendea wema wazazi wawili baada ya kufa kwako, nao ni katika wema ambao mtoto anafaidika nao.
- Dua inamnufaisha maiti hata kama haikutoka kwa mtoto, lakini katajwa mtoto pekee kwa sababu ndiye atakayeendelea kumuombea dua mtu mara nyingi mpaka kufa kwake.