- Muislamu anatakiwa kujenga mambo yake juu ya yakini na kuacha yenye kutia shaka ndani yake, na awe na utambuzi katika dini yake.
- Katazo la kutumbukia katika matamanio mabaya.
- Ukitaka utulivu na raha achana na mambo yanayokutia shaka na kuyatupilia mbali.
- Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, pale alipowaamrisha katika mambo ambayo ndani yake kuna raha ya moyo, na akawakataza katika yale yanayotia msongo na utata.