- Dhambi kubwa kabisa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu; kwa sababu amelifanya kuwa dhambi kubwa la kwanza na kubwa kuliko yote, na inayotia mkazo katika hili ni kauli yake Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi pale anaposhirikishwa, na anasamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye".
- Ukubwa wa haki ya wazazi wawili, pale alipoambatanisha haki zao na haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Madhambi yanagawanyika makubwa na madogo, na dhambi kubwa ni: Kila dhambi lenye adhabu duniani, kama kusimamishiwa sheria na laana, au ahadi ya adhabu ya Akhera, kama ahadi ya adhabu ya moto, pia madhambi makubwa yana daraja, baadhi yake ni mazito kuliko mengine katika uharamu, na madhambi madogo nayo ni yale yasiyokuwa makubwa.