- Uharamu wa kumuua aliyechukua ahadi ya amani na kafiri anayeishi na waislamu, na aliyeomba amani katika makafiri, nakuwa jambo hilo ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.
- Aliyechukua ahadi: Ni kafiri aliyechukua ahadi ya kutowapiga vita waislamu na huku akiishi katika mji wake, na wao wasimpige vita, na dhimi: Ni yule anayeishi mji wa waislamu na akalipa jizia (kodi ya kichwa), na muomba amani: Ni mtu aliyeingia mji wa waislamu kwa mkataba na amani kwa muda maalumu.
- Tahadhari ya kufanya hiyana katika makubaliano na wasiokuwa waislamu.