- Sheria ya kuleta talbiya (muitikio) katika Hija na Umra, na mkazo wake ndani yake; kwa sababu hiyo ndiyo nembo yake maalumu, kama ambavyo takbiri (Allaahu Akbar) ni nembo ya swala.
- Amesema bin Munir: Na katika sheria ya talbiya kuna ukumbusho juu ya ukarimu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake kuwa misafara yao kwenda katika Al-kaaba ilikuwa ni kwa wito maalum kutoka kwake Aliyetakasika na kutukuka.
- Kilicho bora ni kushikamana na talbiya ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hakuna tatizo kuongeza, kwa kukiri kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hilo, amesema bin Hajari: Na hii ndio namna ya uadilifu zaidi, kwa kusema pekee maneno yalikuja kwa kuchukuliwa moja kwa moja kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akichagua kauli iliyokuja kutoka kwa swahaba pekee, au akaanzisha mwenyewe katika yale yanayofaa, yeye mwenyewe peke yake ili maneno yasichanganyike na yale yaliyonukuliwa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hii inafanana na hali ya dua katika tahiyatu, kwani alisema katika dua hiyo: Kisha achague katika maombi na sifa azitakazo: Yaani baada ya kumaliza ile iliyofundishwa.
- Sunna ya kunyanyua sauti katika talbiya, na hii ni kwa wanaume, ama mwanamke atashusha sauti yake kwa kuhofia fitina.