- Kiapo cha uongo hakina kafara; kwa ubaya wa hatari yake, bali kinatoba.
- Kuishia kutaja madhambi makubwa haya manne katika hadithi ni kwa sababu ya ukubwa wa dhambi zake, na si kwa kudhibiti idadi yake.
- Madhambi yanagawanyika makubwa na madogo, na dhambi kubwa ni: Kila dhambi lenye adhabu duniani, kama kusimamishiwa sheria na laana, au ahadi ya adhabu ya Akhera, kama ahadi ya adhabu ya moto, pia madhambi makubwa yana daraja, baadhi yake ni mazito kuliko mengine katika uharamu, na madhambi madogo nayo ni yale yasiyokuwa makubwa.