- Kukata udugu ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.
- Kuunga udugu kunakuwa kulingana na desturi za watu, na kutatofautiana kulingana na mazingira na zama na jamii pia.
- Kuunga udugu kunakuwa kwa kutembeleana, na kwa sadaka, na kuwatendea wema, na kuwatembelea wagonjwa, na kuwaamrisha mema, na kuwakataza maovu, na mengineyo.
- Kila ambavyo kukata udugu kunavyozidi kuwa kwa ndugu wa karibu zaidi ndivyo ambavyo madhambi yanavyokuwa makubwa.