- Ni haramu kutoa rushwa, na kuichukua, na kuwa wakala wake, na kusaidia; kwa sababu ndani yake kuna kusaidizana katika batili.
- Rushwa ni katika madhambi makubwa; kwa sababu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kamlaani mpokeaji wake na mtoaji wake.
- Rushwa katika mlango wa kesi na hukumu ni dhulma kubwa na ni dhambi kubwa mno; kwani hapa kuna dhulma na kuhukumu kwa yale ambayo hakuyateremsha Mwenyezi Mungu.