- Ndugu wa karibu ni wale wa upande wa baba na mama, na kadiri anavyokuwa wa karibu zaidi ndivyo anavyokuwa bora zaidi kwa kuungwa udugu.
- Malipo huendana na matendo, atakayeunga udugu wake kwa wema na ihisani, naye pia Mwenyezi Mungu atamuunga katika umri wake na riziki yake.
- Kuunga udugu ni sababu ya kukunjuliwa riziki na kupanuliwa kwake, na ni sababu ya umri mrefu, hata kama kifo na riziki vina muda maalum isipokuwa hili linaweza kuwa ni baraka katika riziki na umri, akafanya mengi katika umri wake na yenye manufaa zaidi kuliko atakavyofanya mwingine, na wanasema wanachuoni; ziada katika riziki na umri ni zaida ya uhalisia. Na Allah ndiye Mjuzi zaidi.