- Mazungumzo haya ni katika kumtanguliza mama, kisha baba, kisha ndugu wa karibu zaidi na wa karibu anayefuata, kulingana na daraja zao katika ukaribu.
- Kumebainishwa nafasi ya wazazi wawili na hasa hasa mama.
- Amekariri katika hadithi wema kwa mama mara tatu; na hii ni kwa sababu ya ukubwa wa fadhila yake kwa watoto wake, na kwa sababu ya wingi wa matatizo anayovumilia na tabu na uzito wa ujauzito, kisha kujifungua, kisha kunyonyesha, mambo ambayo yako kwake pekee, kisha baba anashiriki katika malezi.