Imepokewa kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haingii peponi mfitinishaji".
Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Ufafanuzi
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mmbea anayehamisha maneno kati ya watu kwa lengo la kuwavuruga kati yao yakuwa anastahiki adhabu kwa kutoingia peponi.
Hadeeth benefits
Umbea ni katika madhambi makubwa.
Katazo la umbea; kwani ndani yake kuna kuwavuruga watu na madhara baina ya mtu na mtu na jamii mzima.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others