- Dhana mbaya haidhuru kwa mtu ambaye zimedhihiri kwake alama zake, na ni wajibu juu ya muumini awe mwerevu mjanja, hadanganyiki na watu waovu na mafasiki.
- Makusudio yake ni kutahadharisha na tuhuma ambazo zinabakia ndani ya nafsi, na kuziendeleza, ama yanayojitokeza ndani ya nafsi na hayabakii haya mtu hachukuliwi katenda dhambi.
- Kuchukua tahadhari dhidi ya sababu za kubezana na kukata mahusiano baina ya jamii ya kiislamu, ikiwemo ujasusi na husuda na mfano wake.
- Usia kwa muislamu wa kuamiliana na ndugu yake muamala wa ndugu kwa ndugu katika nasaha na mapenzi.