- Amri ya kutekeleza jambo lolote linalopelekea udugu wa kiimani, na katazo la kufanya kinyume chake miongoni mwa kauli na vitendo.
- Nguzo ya ucha Mungu ndani ya moyo ni kumtambua Mwenyezi Mungu, na kumuogopa na kumchunga, una ucha Mungu huu ndio unaozaa matendo mema.
- Kupinda kwa wazi kunaonyesha udhaifu wa ucha Mungu wa moyo.
- Katazo la kumuudhi muislamu kwa aina yoyote ile, kwa kauli au kitendo.
- Si katika husuda muislamu kutamani awe kama mwenzake, bila kutamani neema hiyo iondoke kwa mwenzake, na hii huitwa kufurahia neema ya mwenzio (na kuitamani pia uipata); na hii inafaa, kwani inasaidia watu kushindana katika mambo ya kheri.
- Mwanadamu katika tabia zake hapendi yeyote amzidi katika chochote miongoni mwa fadhila, ikiwa atapenda iondoke neema hiyo kwa mwenzake hiyo itakuwa ni husuda mbaya, na ikiwa atapenda kushindana basi hiyo inaitwa kufarahia neema kunako faa.
- Si katika kuuza muislam juu ya biashara ya ndugu yake kwa kumuweka wazi mteja kuwa kadanganywa katika kununua tena uongo mbaya; bali hili ni katika sehemu ya nasaha, kwa sharti iwe matokeo yake ni kumnasihi ndugu yake mnunuzi, na si kumdhuru muuzaji, kwani matendo huhukumiwa kwa nia.
- Si katika kuuza muislamu juu ya biashara ya ndugu yake ikiwa muuzaji na mnunuzi hawajakubaliana na wala kiwango cha thamani hakijapitishwa.
- Si katika kuchukiana kuliko katazwa ndani ya hadithi: Kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, bali hilo ni wajibu, na ni katika misingi mizito ya imani.