- Sababu ya kuharamishwa pombe ni kilevi, hivyo, kila chenye kulevya kiwe kwa aina yoyote ile ni haramu.
- Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha pombe; kwakuwa imekusanya madhara na maovu makubwa.
- Kunywa pombe peponi ni katika ukamilifu wa ladha na utimilifu wa neema.
- Ambaye hakuizuia nafsi yake na unywaji pombe duniani Mwenyezi Mungu atamharamishia kuinywa peponi, kwani malipo huendana na matendo.
- Hili ni himizo la kufanya haraka kutubia dhidi ya madhambi kabla ya kifo.