- Ukubwa wa swala la kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuwi ila kwa haja.
- Kipato cha haramu hata kama kitakuwa kingi; basi hicho kimeondolewa baraka wala hakina kheri ndani yake.
- Amesema Qaari: Kuondoka kwa baraka za kipato; ima kwa uharibifu unaoweza kutokea katika mali yake, au kwa kuitoa katika mambo ambayo hanufaiki nayo katika dunia au thawabu Akhera, au zikabakia kwake lakini akanyimwa kunufaika nazo, au akazirithi ambaye hatomshukuru.
- Amesema Nawawi: Hapa kuna katazo la kukithirisha kuapa katika biashara, kwa sababu kuapa pasina haja ni machukizo, na linaambatana hilo na kupambia bidhaa, na huenda mnunuzi akadanganyika na kiapo.
- Kukithirisha viapo ni upungufu wa imani, na ni upungufu wa tauhidi; kwa sababu kukithirisha viapo kuna pelekea mambo mawili: La kwanza: Kupuuza hilo na kutojali, la pili: Uongo, kwa sababu mwenye kukithiri viapo vyake huingia katika uongo, ni lazima kupunguza na kutokithirisha viapo, na ndio maana alisema Mtukufu: "Na hifadhini viapo vyenu" [Maaida: 89].