- Amesema Imam Nawawi: Hii ni kanuni endelevu katika Sheria, kuwa kila jambo la heshima na utukufu kama vile kuvaa nguo, suruali, kandambili, kuingia msikitini, kupiga mswaki, kupaka wanja, kukata kucha, kupunguza masharubu, kuchana nywele, kung'oa nywele za kwapa, kunyoa kichwa, kutoa salam ya kumaliza swala, na kuosha viungo kwa ajili ya usafi, na kutoka nje ya choo, kula na kunywa, kupeana mikono, kugusa Jiwe Jeusi, na mambo mengine yenye kufanana na haya, basi ni sunna kuanza na upande wa kulia, na ama yale yaliyo kinyume chake, kama vile kuingia chooni, kutoka msikitini, kukidhi haja ndogo, kujisafisha, kuvua nguo, suruali, kandambili, na kadhalika, haya ni sunna kuanza na upande wa kushoto, na yote hayo ni kwa sababu ya heshima ya upande wa kulia na utukufu wake.
- "Anapendezwa na kuanzia kulia" Inajumuisha: Kuanza vitendo kwa mkono wa kulia, mguu wa kulia, upande wa kulia, na kushughulikia kitu kwa mkono wa kulia.
- Amesema Imam Nawawi: Tambueni kuwa miongoni mwa sehemu za udhu kuna ambazo hazipendezi kuanzia kulia; ambazo ni masikio, viganja, na mashavu, bali vitasafishwa vyote kwa wakati mmoja, ikiwa halitowezekana hilo kama ilivyo kwa mtu aliyekatwa sikio na mfano wake; basi atatanguliza upande wa kulia.