Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayekula kitunguusaumu, a...
Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekula kitunguu saumu au kitunguu maji asije msikitini, ili asiwaudhi ndugu zake katika wale wanaoh...
Kutoka kwa Sahal bin Muadhi bin Anas kutoka kwa baba yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayekula chakula, akasema: Kila si...
Anamhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kula chakula amshukuru Mwenyezi Mungu, kuwa mimi sina uwezo wa kuleta chakula wala kukila isipok...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au n...
Alikuwa rehema na amani ziwe juu yake anapopiga chafya:
Jambo la kwanza: Anaweka mkono wake, au nguo yake juu ya kinywa chake; Kisije kutoka kinywa...
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kw...
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kuwa Mwenyezi Mungu anapenda ziendewe ruhusa zake ambazo ameziweka, ikiwemo kufanya wepesi katika...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwenye kutakiwa kheri na All...
Anaeleza Mtume -Rehama na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu akitaka kheri kwa yeyote katika waja wake waumini huwapa mtihani katika nafsi zao...
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayekula kitunguusaumu, au kitunguu maji, basi na ajitenge nasi, au ajitenge na msikiti wetu, na akae nyumbani kwake", Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliletewa chungu kikiwa na mbogamboga, akakuta zinaharufu, akauliza akaelezwa kilichomo katika mboga hizo, akasema: Wapewe baadhi ya Maswahaba zake aliokuwa nao, alipoiona hakupendezwa nayo, akasema: "Kula kwani mimi ninanong'ona na yule usiyenong'ona naye".
Kutoka kwa Sahal bin Muadhi bin Anas kutoka kwa baba yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayekula chakula, akasema: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki, na akaniruzuku, si kwa ujanja wangu wala kwa nguvu zangu, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia".
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza sauti yake.
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu anapenda ichukuliwe ruhusa yake katika kufanya yaliyo mepesi, kama vile anavyopendelea kwa waja wake kufanya mambo yake aliyowawajibishia kuyafanya".
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwenye kutakiwa kheri na Allah, (Allah) humuonja kutokana na kheri hiyo.
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry na kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haumpati muislamu uchovu wala maradhi, wala msongo, wala huzuni, wala udhia, wala shida, hata mwiba unaomchoma, isipokuwa anamfutia Mwenyezi Mungu kupitia hilo makosa yake."
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Majaribio hayaachi kumpata muumini wa kiume na muumini wa kike katika nafsi yake, na watoto wake, na mali yake mpaka atakapokutana na Mwenyezi Mungu ilhali hana dhambi hata moja."
Kutoka kwa Suhaib -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini, akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake."
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Pindi anapougua mja au akasafiri basi huandikiwa mfano wa yale aliyokuwa akiyafanya akiwa nyumbani tena mwenye afya".
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama kipande cha usiku wa giza, anaamka mtu akiwa muislamu anafika jioni akiwa kafiri, na anashinda akiwa muumini anaamka asubuhi akiwa kafiri, anauza dini yake kwa thamani ndogo ya dunia"
Imepokewa kutoka kwa Muawiya -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Mwenye kutakiwa kheri na Allah humpa ufahamu katika dini, mimi ni mgawaji tu, na Allah ndiye anayetoa, na umma huu utaendelea kusimama katika amri ya Mwenyezi Mungu, hatowadhuru mwenye kuwapinga, mpaka ije amri ya Mwenyezi Mungu".
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote akakifikisha kama alivyo sikia, huenda mfikishiwa akawa mwerevu zaidi kuliko aliye sikia".