- Fadhila ya kushukuru nyakati za kheri na kuwa na subira wakati wa dhiki, mwenye kufanya hivyo atapata kheri zote za Dunia na Akhera, na asiyeshukuru juu ya neema, na wala havumilii juu ya msiba atakosa ujira na kupata mzigo (wa dhambi).
- Fadhila ya Imani, na kwamba malipo kwa kila hali ni kwa watu wenye imani.
- Kushukuru nyakati za kheri na subira wakati wa shida ni miongoni mwa sifa za waumini.
- Kuamini maamuzi na Kadari za Mwenyezi Mungu humfanya Muumini kuridhika kabisa na hali zake zote, tofauti na kafiri ambaye hukasirika mara kwa mara pindi anapopatwa na madhara, na akipata neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu huacha kumtii Mwenyezi Mungu, na huenda mbali zaidi na kuzitumia katika kumuasi.