- Himizo la kuhifadhi mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kuyafikisha kwa watu.
- Kumebainishwa fadhila za watu wa hadithi, na heshima ya kuitafuta kwake.
- Fadhila ya wanachuoni, ambao wanastahiki kuchambua na kuzielewa hadithi.
- Ubora wa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, wao ndio waliosikia hadithi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wakatufikishia.
- Amesema Al-Munaawi: Amebainisha kuwa mpokezi wa hadithi kuwa na uelewa si katika sharti zake, bali sharti lake ni kuhifadhi, na kwa msomi kuelewa na kuzingatia.
- Amesema bin Uyaina: Hakuna yeyote anayetafuta hadithi isipokuwa kuna mng'ao katika uso wake kwa hadithi hii.
- Kuhifadhi kwa wasomi wa hadithi kuna aina mbili: Kuhifadhi kwa moyo na kifua, na kuhifadhi kwa kitabu na mwandiko, na aina zote mbili zinakusanywa na dua iliyoko katika hadithi.
- Ufahamu wa watu unatofautiana, huenda mfikishiwa akawa muelewa zaidi kuliko aliyesikia, na huenda aliyebeba maarifa ya sheria akawa si muelewa.