Pindi anapougua mja au akasafiri basi huandikiwa mfano wa yale aliyokuwa akiyafanya akiwa nyumbani tena mwenye afya
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Pindi anapougua mja au akasafiri basi huandikiwa mfano wa yale aliyokuwa akiyafanya akiwa nyumbani tena mwenye afya".
Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Ufafanuzi
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu fadhila za Allah na rehema zake, nakuwa muislamu ikiwa ni katika mazoea yake kufanya matendo mema akiwa katika hali ya afya na yuko nyumbani, kisha apatwa na udhuru akaugua akashindwa kutekeleza ibada hizo, au akashughulishwa na safari, au udhuru wowote; basi huandikiwa malipo kamili, kama ambavyo angefanya wakati wa afya na yuko nyumbani.
Hadeeth benefits
Upana wa fadhila za Allah kwa waja wake.
Himizo la kuongeza juhudi katika ibada na kutumia fursa ya nyakati za afya na wasaa.
Share
Use the QR code to easily share the message of Islam with others