- Inapendeza kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu mwisho wa chakula.
- Kuna ubainifu wa fadhila kubwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya waja wake, kwa kuwa amewaruzuku na kuwasahilishia riziki, na akalifanya hilo kuwa ni kafara ya kusamehewa madhambi.
- Mambo ya waja yote yanatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na si kwa uwezo wao au nguvu zao, na mja ameamrishwa kufanya sababu.