- Katazo la kuja msikitini kwa atakayekula kitunguu saumu, au kitunguu maji, au chochote chenye harufu mbaya.
- Inaunganishwa na mambo haya, kila chenye harufu mbaya kinachowakera wenye kuswali, kama harufu ya sigara na tumbaku ugoro na mfano wa hivyo.
- Sababu ya kukatazwa ni harufu, ikiondoka kwa kupikwa sana au kwa kinginecho; basi chukizo litaondoka.
- Chukizo la kula vitu hivi kwa mwenye ulazima wa kuhudhuria swala msikitni; ili jamaa isimpite msikitini, madam hajavila kwa hila ya kukwepa kuhudhuria swala ya jamaa, hapa itakuwa ni haramu.
- Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukataa kula kitunguu saumu na mfano wake, si kwa ajili ya kuharamisha, bali ni kwa sababu ya mazungumzo yake na Jibril amani iwe juu yake.
- Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba hukumu anaiambatanisha na sababu yake; ili mkusudiwa atulizane kwa kujua hekima.
- Amesema Al-qadhi: Na wanachuoni wametumia kipimo hiki kwa maeneo yote yanayowakusanya watu kwa ajili swala kama viwanja vya Idd na jeneza na mfano wake katika sehemu zinazowakusanya watu kwa ajili ya ibada, na vile vile sehemu wanazokusanyika kwa ajili ya elimu na kumtaja Mwenyezi Mungu na sherehe mbali mbali na mfano wake, isipokuwa masoko na mfano wake hayaingii hapa.
- Wamesema wanachuoni: Na katika hadithi hii kuna dalili ya kukataza kula kitunguu saumu na mfano wake wakati wa kuingia msikitini, hata kama pakiwa hakuna mtu ndani yake, kwa sababu ni mahala pa Malaika, na kwa ujumla wa maelekezo ya hadithi.