Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akimtaja Allah katika nyakati zake zote.
Anaeleza Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa na pupa kubwa ya kumtaja Allah Mtukuf...
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna kitu kinachotukuzwa...
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna chochote katika ibada kilicho bora zaidi mbele ya Allah Mtukufu kuliko dua; kwa sababu n...
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna muislamu ye...
Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa muislamu atakapomuomba Mwenyezi Mungu na akamuomba maombi ambayo si dhambi, kama kumuomba amrahisis...
Kutoka kwa Ubaada bin Swaamit radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Peponi kuna daraja mia moja b...
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa peponi kuna daraja na vituo mia moja, na masafa yaliyopo kati ya daraja mbili ni kama masafa kati ya...
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara...
Dua nyingi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake zilikuwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu uthabiti katika dini na utiifu, na kujiepusha na kupinda na upot...

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akimtaja Allah katika nyakati zake zote.

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna kitu kinachotukuzwa zaidi kwa Allah Mtukufu kuliko dua".

Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna muislamu yeyote ataomba maombi yasiyokuwa ndani yake na kuomba dhambi wala kukata udugu, isipokuwa Allah atampa kwa maombi hayo moja kati ya mambo matatu: Moja ima amuharakishie maombi yake, au amlimbikizie ili amlipe siku ya Kiyama, au amuondoshee katika mabaya mfano wake" Wakasema: (Maswahaba) kwa hiyo tuzidishe? Akasema: "Allah ni mwenye kuzidisha mara dufu".

Kutoka kwa Ubaada bin Swaamit radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Peponi kuna daraja mia moja baina ya kila daraja mbili ni kama umbali wa mbingu na ardhi, na Firdausi iko daraja ya juu zaidi kuliko zote, na ndani yake ndiko inako chimbuka mito yote minne ya pepo, na juu yake ndiko inakokuwa Arshi, Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi".

Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.” Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunakuamini wewe na ulicholeta, je unatuhofia? Akasema: "Ndio, nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, anazigeuza kwa namna atakavyo"

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu, na unitengenezee dunia yangu ambayo kunapatikana maisha yangu, na unitengenezee Akhera yangu ambako kunapatikana kuishi kwangu milele, na unijalie ziada ya uhai kwenye kila lenye heri, na ujalie kifo ni kitulizo changu kutokana na kila shari"

Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiacha dua hizi, kila anaposhinda jioni na kila anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba msamaha na afya katika dini yangu na dunia yangu na familia yangu na mali yangu, ewe Mwenyezi Mungu sitiri uchi wangu -Au aibu zangu- na utie amani yote ninayoyahofia, ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi toka mbele yangu, na nyuma yangu, na kuliani kwangu, na kushotoni kwangu, na juu yangu, na ninajilinda kwa utukufu wako nisijekuvamiwa tokea chini yangu".

Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimfundisha dua hii: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka na za kuchelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua, na ninajikinga kwako kutokana na shari zote zinazokuja haraka na zinazochelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) miongoni mwa heri alizo kuomba mja wako na nabii wako, na ninajikinga kwako (uniepushe) na shari alizo jikinga kwako mja wako na nabii wako. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba pepo, na yaliyo karibu yake miongoni mwa kauli au matendo, na ninajikinga kwako kutokana na moto na yaliyo karibu na moto miongoni mwa kauli au matendo, na ninakuomba ujaalie kila hukumu utakayo hukumu kwangu iwe ni heri"

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Umar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Imani huoza na kudhoofika kwenye mwili wa mmoja wenu kama inavyooza nguo mpya kwa kukaa muda mrefu, basi muombeni Mwenyezi Mungu aifanye Imani kuwa mpya kwenye nyoyo zenu."

Kutoka kwa Abbasi bin Abdil Muttwalib radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Amekwisha ionja ladha ya imani, yule mwenye kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola wake, na Uislamu ndiyo dini, na Muhammad ni Mtume"

Kutoka kwa Muadhi bin Jabali -radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimshika mkono wake, na akasema: "Ewe Muadhi, Wallahi hakika mimi ninakupenda", Akasema: "Ninakuusia ewe Muadhi usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni ibaadatika" Ewe Mwenyezi Mungu nisadie katika kukutaja na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako".

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu,Basi zidisheni dua".