- Kudumu na maneno haya kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Mwanadam kama alivyo anaamrishwa kumuomba Mwenyezi Mungu afya katika dini, vile vile kaamrishwa kumuomba katika dunia.
- Amesema Attwayibi: Imekusanya pande zote sita; kwa sababu maafa mengi hutokea katika pande hizo, na akatia mkazo katika upande wa chini kwa sababu maafa ya kutoka chini huwa mabaya zaidi.
- Kilicho bora wakati wa kusoma Adhkari, wakati wa asubuhi: Ni kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuchomoza Jua mwanzo wa mchana, na kuanzia baada ya Lasiri mpaka kabla ya Maghribi, ikiwa atasema baada ya wakati huo, yaani: Akazisoma asubuhi baada ya Jua kunyanyuka itafaa pia, na hata akisema baaada ya Adhudhuri itamfaa pia, na ikiwa atazazisema baada ya Maghrib itamtosheleza pia, huo ndio wakati wa kufanya dhikri.
- Dalili ikionyesha kuwa dhikri inamuda maalum wakati wa usiku kama kusoma aya mbili za mwisho katika suratul baqara basi hii inakuwa ni baada ya kuzama kwa Jua.