- Mtu anatakiwa kuifundisha familia yake yale yenye kuwanufaisha katika mambo ya dini na dunia, kama Mtume rehema na amani ziwe juu yake alivyomfundisha Aisha.
- Kilicho bora kwa muislamu ni kuhifadhi dua zilizopokelewa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake; kwa sababu ni katika dua zilizokusanya kheri zote.
- Wanachuoni wanasema kuhusu hadithi hii: Ni hadithi iliyokusanya kila kitu katika kuomba kheri na kuomba kinga dhidi ya shari, hii ni katika maneno mafupi yenye maana pana aliyopewa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Miongoni mwa sababu za kuingia peponi baada ya rehema ya Mwenyezi Mungu: Ni matendo na kauli njema.