- Kujisalimisha kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Mola wake Mlezi na kunyenyekea kwake, na kuuelekeza umma kuliomba hilo.
- Umuhimu wa kuwa na msimamo na uthabiti katika dini, na kuwa kinachozingatiwa ni hatima ya mtu ya maisha yake.
- Mja hawezi kujitosheleza mwenyewe hata kwa kupepesa jicho bila ya kutiwa uthabiti na Mwenyezi Mungu katika Uislamu.
- Himizo la kuomba dua hii kwa wingi, kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Kudumu katika Uislamu ni neema kubwa ambayo mja anatakiwa kuifanyia juhudi na kumshukuru Mola wake Mlezi.