- Kutofautiana kwa vituo vya watu wa Peponi, na hii ni kulingana na imani na mtendo mema.
- Himizo la kumuomba Mwenyezi Mungu Firdausi ya juu katika Pepo.
- Firdausi ndiyo Pepo ya juu, na ndio bora zaidi kuliko zote.
- Ni wajibu kwa muislamu hamu yake kuwa ya juu zaidi, na aende mbio na aombe makazi ya juu na bora zaidi kuliko yote mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Mito minne ya Pepo ni mito ya maji na maziwa na mvinyo na asali iliyotajwa ndani ya Qur'ani katika kauli yake Mtukufu: "Mfano wa Pepo waliyoahidiwa wachamungu, ndani yake kuna mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isiyoharibika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa" [Muhammadi: 15].