- Dua ya muislamu hujibiwa hairejeshwi lakini kwa sharti zake na adabu zake; ndio maana inampasa mja akithirishe dua na wala asitake haraka ya kujibiwa.
- Kujibiwa dua hakufungamani na kupata kilichoombwa; kwani anaweza kumfutia madhambi kwa dua yake, au akamlimbikizia Akhera.
- Amesema bin Bazi: Kung'ang'ania, na kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu, na kutokata tamaa, hizi ni miongoni mwa sababu kubwa za kujibiwa, ni juu ya kila mtu kung'ang'ania katika dua, na awe na dhana nzuri na Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka, na ajue kuwa yeye ni mwenye hekima na mjuzi, anaweza kuharakisha majibu kwa hekima, na anaweza kuyachelewesha kwa hekima, na anaweza kumpa muombaji kitu bora kuliko alichoomba.