- Sheria ya kumueleza mtu kuwa unampenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
- Inapendeza kuomba dua hii mwisho wa kila swala ya faradhi na ya sunna.
- Katika kuomba kwa matamshi haya machache kuna mahitaji yote ya Dunia na Akhera
- Katika faida za kupendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kuusiana katika na kupeana nasaha katika mambo mema na uchamungu.
- Amesema Attwayibi: Kumtaja Mwenyezi Mungu ni utangulizi wa kukunjua kifua, na kumshukuru ni njia ya kuzilinda neema, na kuzifanya vizuri ibada ni kujiweka mbali na yote yanayomshughulisha mtu na Mwenyezi Mungu Mtukufu.