- Ubora wa dua nakuwa mwenye kumuomba Allah basi huwa kamtukuza, na amekiri kuwa Yeye ni mkwasi -Aliyetakasika- kwani Masikini haombwi, nakuwa Yeye ni Msikivu, kwani kiziwi haombwi, nakuwa Yeye ni mkarimu, kwani bahili haombwi, nakuwa yeye anahuruma, kwani mkorofi haombwi, nakuwa Yeye anaweza, kwani asiyejiweza haombwi, nakuwa Yeye yuko karibu, kwani aliyembali hasikii, na zinginezo katika sifa za utukufu na za uzuri wa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na Kutukuka-.