- Imani ina utamu na ladha inayoonjwa kwa mioyo, kama inavyoonjwa ladha ya chakula na kinywaji kwa mdomo.
- Mwili haupati ladha ya chakula na kinywaji isipokuwa unapokuwa na afya njema, hivyo hivyo hata moyo ukisalimika na maradhi ya matamanio potofu, na matamanio yaliyoharamishwa, utapata utamu wa imani, na utakapougua na nakuwa mgonjwa kamwe hauwezi kupata utamu wa imani, bali unaweza kupata utamu wa mambo yanayoangamiza kama matamanio na maasi.
- Mwanadam atakaporidhia jambo na akaliona kuwa zuri linakuwa jepesi kulifanyia kazi, na wala hakuna kitakachoweza kumpa tabu katika hilo, na atafurahia kwa kila kilichokuja katika jambo hilo, na bashasha itaingia ndani ya moyo wake, hivyo hivyo hata muumini imani inapoingia ndani ya moyo wake, huwa rahisi kwake kumtii Mola wake Mlezi na nafsi yake huhisi ladha, na hakuna tabu zitakazomuwia ugumu.
- Amesema Ibnil Qayyim: Hadithi hii imekusanya kuridhia uumbaji na upangiliaji wake Mtukufu na uungu wake, na kuridhika na Mtume wake na kumtii, na kuridhika na dini yake na kujisalimisha kwa dini hiyo.