- Kumebainishwa fadhila ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake waumini na huruma yake kwao kwa kuwasamehe madhambi hata kwa madhara madogo yanayowasibu.
- Ni lazima kwa muislamu ataraji malipo kwa Allah kwa yale yanayomsibu, na asubiri kwa dogo na kubwa, ili iwe ni sababu ya kunyanyuliwa daraja na ni kafara ya makosa.